• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya reli ya Beijing kusafirisha zaidi ya watu milioni 37 wakati Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina

    (GMT+08:00) 2019-01-21 18:38:27

    Mamlaka ya usafiri wa reli ya Beijing inakadiria kuwa, abiria milioni 34.7 watatumia usafiri wa reli wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ikiwa ni kuanzia leo hadi Machi Mosi.

    Kituo cha treni cha Beijing kinatarajiwa kusafirisha abiria milioni 4.14, ikiwa ni ongezeko la asilimia moja ikilinganishwa na mwaka jana, huku kituo cha treni cha Beijing Magharibi na cha Kusini vikitarajiwa kusafirisha abiria milioni 6.56 na milioni 4.82 wakati wa Sikukuu hiyo.

    Ili kukabiliana na idadi kubwa ya wasafiri, mamlaka ya usafiri wa treni ya Beijing imeongeza idadi ya treni zinazokwenda kwenye maeneo maarufu, ikiwemo mjini Jinan, Changchun, Harbin na Chengdu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako