• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi nchini Kenya waimarisha usalama wakati wakisaka watuhumiwa wa ugaidi

    (GMT+08:00) 2019-01-21 19:16:23

    Polisi nchini Kenya wameimarisha operesheni za usalama nchini humo ili kuwasaka wahusika wa shambulizi lililotokea kwenye hoteli moja jijini Nairobi ambapo watu 21 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

    Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo Charles Owino pia amesambaza picha za watu wanane wanaoshukiwa kupanga shambulizi hilo, na kuwataka wananchi kuwa makini na kutoa taarifa kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu nao pindi wakiona mtu yeyote anayeonekana katika picha hizo.

    Pia Bw. Owino amesema, polisi wanaamini kuwa watuhumiwa hao kwa sasa wako nchini Somalia na wanafanya juhudi kupata vitambulisho bandia vya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako