• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya mambo ya nje ya China yakanusha ripoti za CNN kuhusu yaliyotokea wanawake wa kabila la Wauygur

  (GMT+08:00) 2019-01-22 08:56:39

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, baada ya uchunguzi wa makini, China imethibitisha kuwa ripoti zilizotolewa na Shirika la habari la Marekani CNN kuhusu mwanamke mmoja wa kabila la wauygur aliyefungwa katika gereza la Urumqi kushuhudia vifo vya wanawake wengine tisa wauygur na kifo cha mtoto wake katika hospitali ya watoto ya Urumqi, ni "uongo mtupu wa makusudi".

  China inatoa wito kwa vyombo vya habari kufuata maadili ya uanahabari, kuthamini sifa zao, na kutonukuu wala kutunga habari feki. Pia serikali ya China imewataka baadhi ya wabunge wa Marekani kuheshimu ukweli, kuachana na msimamo wa kiitikadi na mawazo ya Vita Baridi, na kuacha vitendo vya kuchafua na kupotosha sera za China kuhusu mambo ya kidini na utawala wa mkoa wa Xinjiang.

  Hivi karibuni shirika la habari la Marekani limetoa ripoti kuhusu yaliyomkumba mwanamke wa kabla ya Wauygur mwenye jina la Mihrigul Tursun, ambaye alidai kuwa mtoto wake wa kiume alifariki dunia katika hospitali ya watoto wa mji wa Urumqi mwaka wa 2015, na alishuhudia mwenyewe vifo vya wanawake tisa wauygur wakati alipotumikia kifungo katika gereza la Urumqi. Akizungumzia ripoti hiyo, Bibi Hua Chunying amesema,

  "Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na idara husika za Xinjiang, Aprili 21 mwaka 2017, Bibi Mihrigul Tursun aliwekwa kizuizini na polisi wa Xinjiang kwa tuhuma za kuchochea chuki za kikabila na ubaguzi wa kikabila. Kwenye kipindi hicho, Bibi Tursun aligunduliwa kuwa na magonjwa ya kuambukiza, na akaachiwa Mei 10 mwaka huo kutokana na sababu za kibinadamu. Mbali na kuwa kizuizini kwa siku hizo ishirini, Bibi Tursun alikuwa huru katika kipindi alipokuwa nchini China. Kwa mujibu wa rekodi, Bibi Tursun alisafiri mara 11 kati ya China na Misri, Umoja wa falme za kiarabu, Thailand na Uturuki. Kwa ufupi ni kwamba Bibi Tursun hakuwahi kufungwa kwenye gereza la Urumqi, na wala hakuwahi kushiriki kwenye mafunzo ya ufundi kazi kwenye kituo chochote. Kwa hiyo sijui alichodai kuwa 'alishuhudia vifo vya wanawake tisa gerezani' na 'alifungwa na polisi kwenye chumba cha gereza chenye wanawake zaidi ya 50' kinatoka wapi?!"

  Kuhusu kifo cha mtoto wake wa kiume katika hospitali ya Urumqi, Bibi Hua Chunying amesema, Bibi Tursun ana watoto watatu, mtoto mmoja wa kiume mwenye jina la Muezi alipelekwa na Bibi Tursun na wanafamilia wake kwenye hospitali ya watoto ya Urumqi kwa ajili ya matibabu mara tatu katika mwaka 2016, na aliondoka China na Bibi Tursun mwezi Aprili mwaka 2018. Mwana wake wa pili anayeitwa Muaizi hakuwahi kuandikishwa nchini China, na pia aliondoka China na Bibi Tursun kwenda nchini Uturuki mwezi Januari mwaka 2016. Kwa hivyo ripoti hiyo kuhusu kifo cha mtoto wa Bibi Tursun katika hospitali ya watoto ya Urumqi haina msingi wowote, na ni uongo mtupu wa makusudi.

  Akiongea kwenye mkutano na wanahabari, Bibi Hua Chunying amesema ukweli ni roho ya uanahabari, na ripoti hiyo ya CNN ni mfano mpya wa habari feki. China inavitaka vyombo vya habari vifuate kwa makini maadili ya uanahabari, kuthamini sifa zao, na kutonukuu na wala kutotunga habari feki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako