• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yakanusha taarifa ya Video ya CCTV Afrika inayosambazwa kuhusu hatari ya usalama Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-01-22 09:28:54

    Msemaji wa serikali ya Tanzania Dk Hassan Abbas amesema video ya CCTV-Afrika inayosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wa viashiria vya kundi la Al Shabaab nchini Tanzania si sahihi na imepitwa na wakati.

    Dk Abbas amesema wamewasiliana na CCTV-Afrika waliotengeneza video hiyo, na kutambua kuwa ripoti yao ilitengenezwa mwaka 2016 kwa mujibu wa ripoti yenye kurasa 53 iliyoandaliwa na jumuiya ya kiserikali ya maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki IGAD, ambayo hata hivyo haikujikita kwenye utafiti wa moja kwa moja nchini Tanzania, zaidi ya hisia za watu wa makundi mbalimbali nchini Kenya, Ethiopia na Somalia.

    Dk. Abbas amesema video hiyo inaenezwa na watu wenye nia mbaya, na kusema tayari CCTV-Afrika wameondoa video hiyo kwenye tovuti yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako