• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CAF yatangaza droo ya hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika

  (GMT+08:00) 2019-01-22 10:14:53

  Timu za Zambia, Zesco na Nkana FC zimepangwa katika kundi C kombe la shirikisho barani Afrika baada ya droo kufanyika jana makao makuu ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) mjini Cairo Misri.

  Timu nyingine katika kundi hilo ni Al Hilal ya Sudan na Asante Kotoko ya Ghana.

  Mabingwa watetezi Raja Club Athetic wamepangwa pamoja na wapinzani wao wa Morocco RS Berkane, Hassania Agadir, na AS Otoho ya DRC kwenye kundi A.

  Kundi B ina timu za Etoile Du Sahel na CS Sfaxien za Tunisia pamoja na Enugu Rangera ya Nigeria na Salitas ya Burkina Faso. Huku kundi D kina timu za Zamalek ya Misri, Gor Mahia ya Kenya, Petro Atletico ya Angola na NA Hussein Dey ya Algeria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako