• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yaanza maandalizi ya AFCON 2019

    (GMT+08:00) 2019-01-22 10:16:57

    Wizara ya michezo ya Misri pamoja na shirikisho la soka nchini humo wametangaza kuanza maandalizi ya mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika yanayoanza Juni 15.

    Waziri wa michezo wa Misri Achraf Sobhi amesema wameshateua kamati zitakazosimamia majukumu mbalimbali ili kuhakikisha maandazili yanakwenda vizuri ikiwemo kamati kuu itakayoongozwa na waziri mkuu na kuwajumuisha mawaziri wote wanaohusiana na mashindano yao.

    Sobhi pia amesema hafla ya ufunguzi na mechi ya kwanza vitafanyika kwenye uwanja wa taifa wa Cairo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 74,000, ambao ulifanyiwa matengenezo kabla Misri haijawa mwenyeji wa michuano ya mwaka 2006.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako