• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kusukuma mbele mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa kazi za kukabiliana na hali ya dharura

  (GMT+08:00) 2019-01-22 18:23:32

  Maofisa wa wizara ya usimamizi wa kazi ya kukabiliana na hali ya dharura wamesema, wizara hiyo iliyoanzishwa mwaka jana imerekebisha idara husika, na imejenga mfumo wa kimsingi wa usimamizi wa kazi za kukabiliana na hali ya dharura wenye umaalumu wa kichina na kuweza kikidhi mahitaji ya zama mpya, na mwaka huu wataendelea kusukuma mbele mageuzi ya mfumo huo, na kupunguza hasara kutokana na maafa kadiri iwezavyo.

  Wizara ya usimamizi wa kazi ya kukabiliana na hali ya dharura ya China ilianzishwa miezi 9 iliyopita, na imebeba majukumu 13 ya idara 11 za zamani. Hadi sasa imejaribu na kujenga utaratibu wa majadiliano kuhusu masuala ya kukabiliana na hali ya dharura, uongozi wa moja kwa moja wa kazi ya uokoaji, na utaratibu wa pamoja wa kazi za kukinga na uokoaji. Aidha, pia imejenga vikosi vya kitaifa vya zimamoto na waokoaji, vikosi 27 vya waokoaji weledi, vikosi 7 vya kimataifa vya waokoaji, na kundi la waokoaji wanaohama. Naibu waziri wa wizara hiyo Bw. Zheng Guoguang anasema,

  "Mwaka jana tuliitikia hali ya dharura mara 47, na kati ya hizo mara 14 ni kwa ajili ya uokoaji wa maafa. Tulituma zaidi ya vikundi 60 vya wafanyakazi wetu, na kutenga dola bilioni 1.7 za kimarekani, mahema elfu 32.8, na mablanketi na nguo zaidi ya laki 4. Hivyo mfumo wetu mpya unaweza kukabiliana na maafa kwa ufanisi mkubwa zaidi, na kuhakikisha vizuri zaidi usalama wa maisha na mali ya wananchi."

  Naibu waziri mwingine wa wizara hiyo Bw. Sun Huashan amesema, wizara hiyo itaendelea kusukuma mbele mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa kazi za kukabiliana na hali ya dharura, na kuweka kipaumbele katika kazi kukinga, kushughulikia na kuokoa. Anasema,

  "Kwa kazi ya kukinga, tutaendelea kufuata mawazo ya kuweka kinga kuwa hatua muhimu zaidi ya kuzuia maafa, na kujenga na kukamilisha mfumo wa kukinga maafa, kuimarisha kuchambua na kutathmini hali ya hatari, na kutunga mpango wa kukabiliana na hali ya dharura. Kwa kazi ya kushughulikia, tutakamilisha mfumo wa kugundua na kushughulikia hatari zilizojificha, na kushughulikia mambo ya usalama katika sekta muhimu, ili kuzuia kutokea kwa ajali na maafa makubwa. Kwa kazi ya uokoaji, tunasisitiza umuhimu wa kuanza kazi hiyo mapema wakati maafa yanapokuwa madogo, na kufahamu vizuri hali ya maafa, ili kupunguza hasara."

  Bw. Zheng amesema vijiji ni sehemu inayoathiriwa zaidi na maafa. Wizara ya usimamizi wa kazi za kukabiliana na hali ya dharura itaongeza nguvu ya kukinga, kupunguza na kuokoa maafa vijijini. Anasema,

  "Tumetoa kipaumbele katika sehemu maskini na zilizoko mbali, na kuhakikisha waokoaji na misaada vinafika kwa wakati, ili kulinda usalama wa maisha na mali ya watu huko."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako