• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: SportPesa 2019: Yanga na Singida United zafungasha virago

  (GMT+08:00) 2019-01-23 09:02:38


  Michuano ya SportPesa imeanza jana jijini Dar es Salaam, Yanga ya Tanzania imeondolewa kwenye mashidano ya kombe la SportPesa kwa kukubali kipigo cha magoli 3-2 toka kwa Kariobangi Sharks ya Kenya na kutupwa nje katika mashindano hayo.
  Mara baada ya kufungwa goli la tatu, kipa wa Kariobangi aling'ang'ania mpira hali ambayo iliwachukiza wachezaji wa Yanga kumpokonya kwanguvu na wachezaji wa Sharks kufika na kuanza ugomvi ambao ulidumu kwa dakika sita baada ya waamuzi watatu kutuliza vurugu hizo.
  Katika mchezo uliotangulia, Singida United nayo imetupwa nje ya michuano hiyo baada ya kuchapwa 1-0 na Bandari ya Kenya.
  Michuano hiyo itaendelea leo kwa mechi nyingine mbili baina ya timu za Tanzania na Kenya, mechi ya kwanza itakutanisha Mbao FC wakimenyana na Gor Mahia mchana na baadaye Simba SC wakiikabili AFC Leopards jioni.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako