• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Russia kufanya ziara Algeria

    (GMT+08:00) 2019-01-23 10:34:59

    Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov leo anaanza ziara ya siku mbili nchini Algeria kufuatia mwaliko wa mwenzake wa Algeria Bw. Abdelkader Messahel. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria imesema ziara ya Bw. Lavrov ni sehemu ya mazungumzo ya kawaida ya kisiasa kati ya nchi hizo mbili. Bw. Lavrov anatarajiwa kufanya mazungumzo na maofisa wa ngazi ya juu wa Algeria ili kubadilishana nao maoni kuhusu masuala makuu ya kikanda na kimataifa ikiwemo hali nchini Libya, Mali na Syria, na suala la kukosekana kwa utulivu kwenye bei ya mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako