• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka 2019 wa Baraza la Uchumi Duniani wafunguliwa Davos, Uswis

    (GMT+08:00) 2019-01-23 10:55:49

    Mkutano wa mwaka 2019 wa Baraza la Uchumi Duniani WEF umefunguliwa mjini Davos, Uswis. Pande mbalimbali zitajadili namna ya kutimiza mafungamano ya kiuchumi yanayozingatia mahitaji ya binadamu. Katika siku ya kwanza kwenye mkutano huo, "China" limekuwa neno linalotajwa mara nyingi zaidi.

    Siku moja kabla ya ufunguzi wa mkutano huo, Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limetangaza ripoti ya makadirio ya uchumi wa dunia, likipunguza makadirio juu ya ongezeko la uchumi duniani katika mwaka 2019 na 2020 kwa asilimia 3.5 na 3.6. Wakati uchumi wa dunia ukizorota kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali, vitendo vya kujilinda kibiashara, utaratibu wa upande mmoja, na siasa zinazojali maoni na fikra za umma zinafufuka katika sehemu mbalimbali duniani. Mwanzilishi wa Baraza la Uchumi Duniani Profesa Klaus Schwab akizungumzia hali hiyo amesema, mafungamano ya kiuchumi duniani ni mwelekeo halisi, utaratibu wa pande nyingi umewasaidia watu mamilioni ya watu kuondokana na umaskini, lakini mchakato huo pia umewafanya baadhi ya watu wawe maskini. Tukikabiliana na changamoto kutokana na mafungamano ya kiuchumi duniani, pande zote zinahitaji kuunganishwa upya, na utandawazi kizazi cha 4.0 unatakiwa kuzingatia zaidi mahitaji ya binadamu, hatua ambayo itakuwa na umuhimu kwa ustawi wa pamoja na mustakbali endelevu wa dunia.

    Wadau na wataalamu 3000 kutoka sekta mbalimbali zikiwemo serikali za nchi, mashirika ya kimataifa, sekta ya biashara, vyuo vikuu, sekta ya utamaduni na vyombo vya habari watafanya majadiliano karibu 400 kuhusu "Mafungamano ya kiuchumi duniani 4.0: kujenga mfumo wa dunia wakati wa zama ya nne ya mapinduzi ya kiviwanda", ili kufanya mawasiliano kuhusu namna ya kujenga mfumo mpya wa jamii shirikishi, na maendeleo endelevu katika dunia yenye utaratibu wa pande nyingi.

    Katika majadiliano kuhusu "Kujikumbusha mgogoro wa kifedha duniani", masuala mbalimbali ya uchumi wa China yakiwemo namna ya kuelewa kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa China, chanzo cha hali hiyo, ufunguaji mlango wa China katika mambo ya fedha, na mustakbali wa madeni, yanafuatiliwa zaidi. Naibu mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Dhamana ya China Bw. Fang Xinghai ameeleza kuwa, kutokana na mgogoro wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, na kupungua kwa kasi ya ongezeko la sekta ya mali zisizohamishika, ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka huu litapungua kiasi, lakini nchini China hali hiyo haioneshi kudorora kwa uchumi. Mwaka 2019 ongezeko la pato la taifa la China GDP linatarajiwa kufikia asilimia 6 ambalo si la kiwango cha chini. Pia ameeleza kama ikiwa uchumi wa China utakabiliwa na changamoto zaidi, China itazidi kuboresha sera mbalimbali za fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako