• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwaka jana serikali ya China ilidumisha uwiano wa mapato na matumizi

    (GMT+08:00) 2019-01-23 17:09:59

    Maofisa wa wizara ya fedha ya China wamesema, mwaka jana kwa mujibu wa sera chanya ya fedha, serikali ilipunguza ushuru na ada kwa nguvu kubwa, huku ikidumisha kiwango cha juu cha matumizi, na hali ya uwiano wa mapato na matumizi ilikuwa nzuri. Wamesema mwaka huu, China itaendelea na sera chanya ya fedha, kuongeza matumizi ya serikali na kupunguza ushuru na ada kwa kampuni na wananchi.

    Naibu mchunguzi wa idara ya akiba ya taifa ya wizara ya fedha ya China Bw. Li Dawei, ameeleza kuwa mwaka jana mapato ya serikali yalifikia dola trilioni 2.65 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 6.2 ikilinganishwa na mwaka 2017. Anasema,

    "Mwaka jana tulitekeleza sera ya kupunguza kodi na ada kwa sekta za uzalishaji, uchukuzi, ujenzi na mazao ya kilimo. Pia tumepunguza ushuru wa watu binafsi. Kutokana na sera hiyo, ongezeko la mapato ya serikali lilipungua kwa asilimia 2.4 ikilinganishwa na mwaka 2017."

    Mchunguzi wa idara ya ushuru ya wizara ya fedha ya China Bw. Xu Guoqiao amesema, mwaka huu serikali itatoa hatua kubwa zaidi ya kupunguza ushuru na ada. Anasema,

    "Tutahimiza zaidi mageuzi ya kodi ya ongezeko la thamani ili kupunguza mzigo wa kampuni, kutekeleza sera iliyorekebishwa ya kodi ya watu binafsi ili kuwapunguzia mzigo wa wananchi, na pia tutatafiti na kutunga mpango wa kupunguza michango ya bima ya kijamii."

    Wakati inapopunguza kodi na ada, serikali ya China imedumisha kiwango cha juu cha matumizi. Naibu mkuu wa idara ya bajeti ya wizara ya fedha ya China Bw. Hao Lei, amesema mwaka jana serikali ilitumia zaidi ya dola trilioni 3.2 za kimarekani kwa ajili ya mambo ya umma, ambalo ni ongezeko la asilimia 8.7 ikilinganishwa na mwaka 2017, na mwaka huu China itaendelea kutekeleza sera chanya ya fedha. Anasema,

    "Kwanza tutaendelea kuongeza matumizi kutokana na hali ya uchumi na mahitaji ya mambo mbalimbali ya umma. Pili tutaongeza shinikizo katika kuboresha mwundo wa matumizi, na kuongeza bajeti kwa juhudi za kuondoa umaskini, mambo ya kilimo, marekebisho ya mwundo wa uchumi, uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, uhifadhi wa mazingira na maisha ya watu. Tatu ni kupunguza matumizi katika mambo ya kawaida, haswa safari za watumishi wa umma katika nchi za nje, magari, na kupokea wageni. Na nne ni kuimarisha usimamzi kwa ufanisi wa matumizi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako