• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utatuzi wa suala la makubaliano ya amani kati Russia na Japan kuchukua muda mrefu

  (GMT+08:00) 2019-01-23 18:52:33

  Rais Vladmir Putin wa Russia amezungumza na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na kusema, makubaliano ya amani kati ya nchi hizo yanahitaji maandalizi ya muda mrefu ili kupata utauzi bora zaidi utakaoridhisha pande zote mbili.

  Rais Putin amesema, kazi muhimu kwa sasa ni kudumisha na kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kwamba makubaliano yatakaofikiwa yanapaswa kuungwa mkono na watu na jamii za pande hizo mbili. Amesema, Russia itaendelea kujitahidi kusukuma mbele shughuli za pamoja na kiuchumi katika kisiwa cha Kuril.

  Kwa upande wake, Bw. Abe amesema, ingawa kuna ugumu mkubwa, lakini suala hilo linapaswa kutatuliwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako