• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Umeme wa kutosha Arusha kuvutia uwekezaji

    (GMT+08:00) 2019-01-23 19:55:23

    Shirika la Umeme nchini (Tanesco), mkoani Arusha, limewaomba wawekezaji kwenda kuwekeza mkoani huko kutokana na kuwa na umeme wa kutosha wa kuendesha viwanda watakavyoanzisha.

    Ombi hilo lilitolewa mkoani humo na Meneja wa Tanesco Arusha, Mhandisi Herini Mhina, akisema kwa sasa wanajitosheleza kwa umeme hivyo wawekezaji wanaokuja kuwekeza mkoani humo watakuwa na uhakika wa nishati hiyo.

    Alisema wafanyabiashara wanapaswa kuunga mkono sera ya viwanda ya awamu ya tano kwa kwenda kuwekeza kwenye nyanja mbalimbali kwa sababu watakuwa na uhakika wa umeme.

    Mhina alisema uwekezaji huo utatoa matokeo chanya kuelekea uchumi wa kati ikizingatiwa hali nzuri ya upatikanaji wa umeme mkoani Arusha ambao ndio mkoa unaoongoza kwenye sekta ya utalii Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako