• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania aagiza wakulima wa korosho walipwe haraka

    (GMT+08:00) 2019-01-24 09:09:50

    Rais John Magufuli wa Tanzania ameziagiza mamlaka husika za Tanzania kuwalipa haraka wakulima wa korosho waliouza korosho zao kwa serikali.

    Akiongea na viongozi wa dini kwenye Ikulu mjini Dar es salaam Rais Magufuli amesema kuna fedha za kutosha na hakuna haja ya urasimu kwenye malipo ya korosho.

    Hata hivyo Rais Magufuli amesema malipo yanatakiwa kulipwa baada ya wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na viongozi wa mashina kwenye mikoa inayolima Korosho ya Mtwara, Lindi, Pwani, Ruvuma na Tanga kuthibitisha malipo hayo.

    Wiki iliyopita waziri wa kilimo wa Tanzania Bw. Japhet Hasunga aliahidi kuwa wakulima hao watalipwa kabla ya mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako