• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yahimizwa kutimiza uwiano wa maendeleo

    (GMT+08:00) 2019-01-24 18:45:50

    Makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan jana alipohutubia mkutano wa mwaka 2019 wa Baraza la Uchumi wa Dunia amesema, utatuzi wa matatizo yaliyotokea kwenye utandawazi wa uchumi unapaswa kulingana na hali halisi, na ukosefu wa uwiano wa maendeleo unapaswa kuondolewa kwa kuhimiza maendeleo zaidi. Baadhi ya wataalamu wanaona kuwa, ukosefu wa uwiano wa maendeleo ni changamoto ya pamoja katika sehemu mbalimbali duniani, na jumuiya ya kimataifa inatakiwa kushirikiana kuhimiza maendeleo zaidi ili kuwanufaisha watu wote duniani.

    Makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan alipohutubia mkutano wa Baraza la Davos la Uchumi wa Dunia amesema, utatuzi wa ukosefu wa uwiano wa maendeleo unategemea maendeleo zaidi, na kuwakosoa watu wengine hakutasaidia. Mwanauchumi mkuu wa Benki ya Zhongyuan ya China Bw. Wang Jun amesema, ukosefu wa uwiano wa maendeleo ni changamoto ya pamoja, na nchi mbalimbali duniani zinapaswa kutatua suala hili kwa kukuza maendeleo zaidi.

    "Hivi sasa tunakabiliwa na ukosefu wa uwiano kati ya nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea, pamoja na ukosefu wa uwiano ndani ya nchi zilizoendelea na ndani ya nchi zinazoendelea. Viongozi wa China wametoa mapendekezo yao ya kutatua suala hilo kwa njia ya maendeleo zaidi."

    Kwenye hotuba yake Bw. Wang Qishan amesema, ili kukabiliana na changamoto, China imechagua njia ya kufanya vizuri mambo yake yenywe. Hivi sasa China pia inakabiliwa na suala la ukosefu wa uwiano wa maendeleo, na tatizo kuu la jamii ya China ni pengo kati ya mahitaji yanayoongezeka ya wananchi kwa maisha bora na hali ya kutokuwa na uwiano wa maendeleo ya kutosha.

    Mwanauchumi maarufu wa China Bw. Zhao Jin amesema China inasukuma mbele mageuzi ya kina ya mwundo wa utoaji, ili kutatua suala la ukosefu wa uwiano wa maendeleo, ili kufanya vizuri mambo yake yenyewe na pia kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya dunia nzima. Anasema,

    "Kuhimiza maendeleo ya mwundo wa utoaji ni kazi yetu kuu kwa sasa. Pia tunasisitiza umuhimu wa kutafuta injini mpya ya maendeleo kutoka kwenye mageuzi. Serikali inapaswa kuongeza nguvu kuunga mkono uvumbuzi wa kampuni na watu binafsi, na kulinda hakimiliki za kiubunifu."

    Kauli mbinu ya mkutano huo ni "utandawazi 4.0, kuanzisha mwundo wa kimataifa wa zama ya mapinduzi ya nne ya kiviwanda". Bw. Wang Qishan amesema teknolojia mpya zinaleta fursa pamoja na changamoto, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuhakikisha usalama wa binadamu, na kujaribu kujenga utaratibu na vigezo husika hatua kwa hatua, licha ya nchi zilizoendelea, pia inapaswa kujali maslahi ya nchi zinazoendelea.

    Bw. Wang Jun anaona kuwa, sayansi na teknolojia zinapaswa kunufaisha binadamu wote, hivyo utaratibu na vigezo husika vinatakiwa kulingana na matakwa ya pande mbalimbali. Anasema,

    "Mapinduzi ya teknolojia yanatoa mchango muhimu kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya binadamu. Wakati duru mpya ya mapinduzi ya teknolojia inapokuja, nchi mbalimbali duniani zinapaswa kufikiria zaidi namna ya kuifanya itoe mchango zaidi kwa binadamu. Tunaona kuwa tunapaswa kuondoa pengo lililoko kati ya nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea kwa kufungua mlango."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako