• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Marekani kuhutubia bunge baada ya idara za serikali kufunguliwa

  (GMT+08:00) 2019-01-24 19:25:30

  Rais Donald Trump wa Marekani atalihutubia bunge kuhusu hali ya taifa baada ya idara za serikali kufunguliwa tena.

  Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, rais Trump amesema atatoa hotuba hiyo baada ya idara za serikali kufunguliwa. Amesema anatafuta sehemu nyingine ya kutoa hotuba hiyo kwa kuwa hakuna eneo linaloweza kushindana na historia, utamaduni na umuhimu wa bunge. Hatua hiyo imekuja baada ya rais Trump na spika wa baraza la chini la bunge la Marekani Nancy Pelosi kutofautiana kuhusu muda na mahali pa kutoa hotuba hiyo.

  Kawaida, hotuba ya hali ya taifa hutolewa kila tarehe 29 Januari, lakini kutokana na idara nyingi za serikali kufungwa, jumatano iliyopita Bi. Pelosi alipendekeza rais Trump kuahirisha tarehe hiyo, akisema kuna hatari ya kiusalama kutokana na kufungwa kwa idara za serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako