• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: SportPesa Cup: Triple C na Njohole wachezaji bora

  (GMT+08:00) 2019-01-25 09:19:48

  Kiungo Mzambia anayekipiga katika klabu ya Simba ya Tanzania Clatous Chota Chama amekabidhiwa hundi na mkurugenzi wa michezi Dkt Yusuf Singo kwa kuwa mchezaji bora katika mechi dhidi ya AFC Leopard ya Kenya kwenye michuano ya SportPesa inayoendelea jijini Dar es Salaam Tanzania. Naye Ibrahim Njohole wa Mbao FC ya Tanzania naye ameibuka mchezaji bora katika mechi dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

  Nusu fainali za mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika leo uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Simba ya Tanzania itakutana na Bandari ya Mombasa Kenya wakati Mbao Fc ya Tanzania yenyewe itakutana na Kariobangi Sharks ya Kenya. Bingwa wa mashindano haya atakutana na Evarton ya Uingereza inayoshiriki ligi kuu ya EPL.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako