• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Chama cha Soka cha Misri chabadilisha ratiba michuano ya AFCON 2019

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:20:48

    Chama cha soka cha Misri (EFA) kimesema hawatatumia uwanja wa Borg Al Arab kwenye mashindano ya AFCON ikitoa sababu kubwa kuwa uwanja huo ni mkubwa sana hivyo itakuwa ngumu sana mashabiki kuujaza.

    Uwanja wa Borg Al Arab upo karibu na Alexandria unaingiza watu 86,000, EFA wamevitaja viwaja vitakavyotumika kuwa ni pamoja na uwanja wa kimataifa wa Cairo, uwanja wa Al-Salaam vyote vipo mjini Cairo, uwanja wa Alexandria, uwanja wa klabu ya Al Masry, uwanja wa klabu ya Ismailia na uwanja wa Suez.

    Chama hicho cha soka wamekiandikia barua chama cha soka Afrika (CAF) kuomba mashindano hayo kuanza Alhamisi tarehe 23 badala ya Ijumaa tarehe 24 mwaka huu na yanajumuisha timu 24 badala ya 16 kama ilivyokuwa awali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako