• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mswada unaoungwa mkono na Rais Trump wa kuidhinisha fedha kwa ajili ya ukuta wa mpakani wakataliwa bungeni

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:28:05

    Mswada unaoungwa mkono na rais Donald Trump wa Marekani ambao unahitaji kuidhinisha fedha kwa ajili ya kujenga ukuta wa mpakani haukupitishwa kwenye baraza la juu la bunge la nchi hiyo.

    Mswada huo uliohitaji kura 60 za kuukubali, uliungwa mkono kwa kura 51 na kupingwa kwa kura 47.

    Mswada mwingine unaoungwa mkono na Chama cha Democrat ili kufunguliwa kwa muda kwa idara za serikali ya Marekani bila ya kuidhinisha fedha za ujenzi wa ukuta, pia umeshindwa kupitishwa kwenye baraza la juu la Marekani.

    Kushindwa kwa miswada hiyo miwili inamaanisha kwamba baraza la juu la bunge la nchi hiyo sasa litahitaji kufanya tena juhudi za kufikia makubaliano juu ya ukuta wa mpakani na kufungua tena idara za serikali ambazo zimefungwa kwa siku 34 hadi sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako