• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Palestina na Israel zakubaliana kumaliza mvutano katika gereza la Ofer

    (GMT+08:00) 2019-01-25 14:12:44

    Wawakilishi wa wafungwa wa Palestina na idara ya magereza ya Israel wamekubaliana kumaliza mvutano wao uliodumu kwa siku tatu katika gereza la Ofer la Israel lililopo Ukingo wa Magharibi. Shirika la Wafungwa la Palestina katika Chama cha Ukombozi wa Wapalestina PLO limesema makubaliano hayo yamefikiwa baada ya majadiliano mfululizo kati ya wawakilishi wa wafungwa na idara ya gereza hilo. Kwa mujibu wa shirika hilo, wafungwa hao waliulazimisha utawala wa gereza hilo kuacha kuwachukulia hatua mbalimbali za adhabu, na kutaka majeruhi watibiwe na kurudisha hali ya kawaida kama ilivyo kuwa kabla ya Januari, 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako