• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Mapinduzi ya vyoo" yaboresha mazingira ya kitalii nchini China

    (GMT+08:00) 2019-01-25 16:59:56

    Kutokana na maendeleo ya teknolojia za kisasa, katika miji na vijiji nchini China, vyoo vimeboreshwa na kuwa safi, vizuri na visivyoleta harufu mbaya na uchafuzi wa mazingira. "Mapinduzi ya vyoo" yameboresha mazingira haswa kwa shughuli za utalii.

    Kisiwa cha Gulangyu kilichoko mjini Xiamen ni sehemu maarufu ya kitalii nchini China. Kila siku zaidi ya watalii 30,000 na wakazi 20,000 wa Xiamen wanatembelea kisiwa hicho. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na matumizi ya teknolojia mpya, baadhi ya vyoo kwa watalii vimeweza kujisafisha kwa kutumia maji machache. Bw. Liu ni mtalii wa huko, anasema,

    "Choo cha hapa ni safi sana, hakuna harafu mbaya yoyote."

    Choo cha Zhaoheshan cha kisiwa hicho kimetumiwa kwa karibu miaka 20. Hivi karibuni kimeimarishwa kwa teknolojia ya kisasa ambayo inashughulikia uchafu kwa kuugawanya kati ya hewa, maji na vitu vigumu

    Mfanyakazi wa idara ya usimamizi wa kazi ya usafishaji ya mji wa Xiamen Bw. Su Feng amesema, imewabidi kujenga chumba cha kuhifadhia mitambo kando ya choo ili kutumia teknolojia hiyo. Anasema,

    "Tunahitajika kujenga chumba cha kuhifadhia mitambo. Licha ya hayo teknolojia hiyo pia inahitaji kiwango cha juu cha utoaji wa umeme."

    Sehemu nyingi maarufu za kitalii nchini China ziko juu ya milima mikubwa. Kwa mfano milima ya Emei na Jiuzhaigou, yote ina mwinuko wa zaidi ya mita 4,000 kutoka usawa wa bahari. Kutokana na tatizo la mwinuko mkubwa, baridi na upungufu wa maji, vyoo vya huko vinatumia zaidi teknolojia ya viumbe.

    Naibu mtafiti wa idara ya utafiti wa viumbe ya mji wa Chengdu ya Akademia ya Sayansi ya China Bw. Zhan Guoqiang amesema, mwaka jana wamejenga choo kimoja katika sehemu ya kitalii ya Niuxinting milimani Emei, ambacho kinatumia teknolojia mpya za kusafisha, na kuongeza joto chooni kupitia vijidudu. Anasema,

    "Tumechagua vijidudu vinavyofaa ambavyo vinaweza kusafisha uchafuzi chooni huku vikiongeza joto. Wakati huo huo, pia tunatumia nishati ya upepo na jua ili kudumisha joto la kuwapendeza watu chooni."

    Hivi saa aina hiyo ya choo imejengwa katika sehemu nyingi za kitalii mkoani Sichuan. Baadaye teknolojia ya akili bandia pia inatarajiwa kutumiwa ili kupunguza nguvukazi kwa kiasi kikubwa.

    Licha ya watalii, wakulima nchini China pia wamenufaika na "mapinduzi ya vyoo". Wanaona kuwa mapinduzi hayo yameleta moja kati ya mabadiliko makubwa zaidi yaliyotokea vijijini katika miaka ya hivi karibuni. Hivi sasa kila nyumba ina choo cha kisasa, na vyoo vya umma pia vimeboreshwa kwa kiasi kikubwa. imefahamika kuwa China itaimarisha "mapinduzi ya vyoo" vijijini kwa kutoa uhakikisho wa fedha na teknolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako