• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 20-January 25)

    (GMT+08:00) 2019-01-25 19:27:22

    Mzozo wa kupanda kwa bei ya mafuta watokota Zimbabwe

    Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amerejea nyumbani baada ya ziara yake nchini Urusi, kufuatia vurugu za maandamano zilizosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.

    Serikali ya Zimbabwe imekuwa ikiulaumu upinzani kutumia hali ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini humo, kuchochea ghasia.

    Aidha upinzani umesema wanachama wake wamekuwa wakichukuliwa hatua kali kama hatua ya kujibu vurugu za maandamano yanayofanywa kupinga ongezeko la mafuta.

    Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic ChangeNelson Chamisa amesema wengi wa wanachama wao wamekamatwa wakiwemo wabunge watano, huku afisa wake mwingine mwandamizi amejificha.

    Amesema vyombo vya ulinzi vimekuwa vikikamata familia za watu majumbani mwao.

    Makundi ya haki za binadamu yanasema kuwa watu 12 wameuawa katika ghasia hizo. Hata hivyo idadi hiyo bado haijathibitisha.

    Jumuia ya Wafanyakazi iliyoitisha maandamano hayo imesema kiongozi wake Japhet Moyo amekamatwa pia.

    Mahakama kuu mjini Harare ilitoa uamuzi kuwa waziri wa serikali hana haki ya kuagiza kufungwa kwa mawasiliano ya internet.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako