• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la juu la bunge la Marekani lazuia miswada miwili katika juhudi za kufungua idara za serikali

  (GMT+08:00) 2019-01-25 20:07:48

  Baraza la juu la bunge la Marekani limezuia miswada miwili inayojaribu kufungua idara za serikali, huku vyama vyote vya siasa vikijitahidi kufikia mwafaka wa kumaliza kufungwa kwa idara hizo ambako kumechukua muda mrefu zaidi katika historia ya nchi hiyo.

  Upigaji wa kura kwa miswada hiyo iliyopendekezwa na Ikulu pamoja na Chama cha Democrats katika siku ya 34 ya kufungwa kwa idara za serikali, haukupata mshindi kwa kuwa hakuna upande uliopata kura 60 za ndio ambazo zinahitajika.

  Moja ya miswada hiyo, uliowasilishwa na chama cha Republican, unataka itengwe dola milioni 5.7 za kimarekani kuwezesha ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako