• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ITU yasema mustakabali wa ushirikiano kati yake na China ni mzuri

    (GMT+08:00) 2019-01-25 20:14:40

    Katibu mkuu wa Shirikisho la Kimatiafa la Mawasiliano ya Simu ITU Bw. Zhao Houlin amesema, sekta ya mawasiliano ya simu ya China imeendelea kwa kasi, na mustakabali wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili ni mzuri.

    Bw. Zhao amesema, baada ya miaka 40 ya utekelezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango, sekta ya mawasiliano ya simu ya China imepata maendeleo makubwa. Hivi sasa, China imekuwa moja ya nchi chache zilizoko mbele zaidi katika uvumbuzi wa teknolojia ya mtandao wa 4G na 5G. Ameongeza kuwa makampuni mengi ya China ya kutengeneza vifaa vya mawasiliano yamekuwa makampuni makubwa ya kimataifa.

    Bw. Zhao pia amesema, tangu mwaka 2015, China, nchi tano za Afrika Mashariki na ITU zimesaini makubaliano kadhaa ya kuongeza ushirikiano. Hivi sasa, shirikisho hilo linazungumza na idara husika za China na nchi za Afrika kutekeleza mpango huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako