• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EABL yaandikisha ongezeko la faida la asilimia 33

    (GMT+08:00) 2019-01-25 20:19:45

    Kampuni ya bia Afrika mashariki EABL imeandikisha ongezeko la faida la asilimia 33 nusu mwaka na kufikia faida jumla ya shilingi bilioni 6.61 . EABL imesema mafanikio hayo yametokana na matokeo mazuri kwenye soko kwenye kila sekta. EABL imesema walifanikiwa kuwekeza katika sehemu nyingi na kuboresha mazingira ya kazi.

    Wakati huo huo kampuni ya kutengeneza simu ya Xiaomi inatarajiwa kufungua ofisi yake ya kwanza mjini Nairobi mwaka huu ikiwa na lengo kuongeza ushindani kati yake na kampuni ya Transsion Holdings inayotengeneza simu za Techno, Infinix na Itel. Hatua hiyo inakuja muda mchache tu baada ya kampuni hiyo kuanzisha idara ya Afrika kwa ajili ya kulenga soko la Afrika ikiwa Kenya. Baadhi ya wachambuzi wa mambo ya biashara wanaona hatua ya kampuni hiyo pia inalenga kupunguza bei ya simu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako