• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu saba wafariki dunia, 150 hawajulikani walipo baada ya bwawa kubomoka nchini Brazil

    (GMT+08:00) 2019-01-26 16:23:15

    Watu tisa wamefariki dunia, tisa wamejeruhiwa na wengine zaidi ya 300 hawajulikani walipo baada ya bwawa linalomilikiwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Vale kubomoka jana mchana katika jimbo la Minas Gerais, Brazil.

    Kwa mujibu wa kampuni ya Vale, wakati ajali inatokea kulikuwa na jumla ya wafanyakazi 427, wafanyakazi 100 waliokuwa wamejitenga waliokolewa, na 300 bado hawajulikani walipo. Idadi ya wahanga inaweza kuwa kubwa zaidi, hasa kutokana na kuwa wakazi wa huo wanaweza kuwa wameathiriwa. Mkuu wa kampuni ya Vale amesema bwawa hilo lilikuwa salama na lilikuwa halitumiki.

    Tayari watu wa idara ya zima moto na waokoaji 100 wamefika kwenye eneo la ajali, na wengine 200 wanatarajiwa kufika leo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako