• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Australian Open 2019: Djokovic amchakaza Nadal fainali

    (GMT+08:00) 2019-01-28 08:27:17
    Mserbia Novak Djokovic ameibuka bingwa wa michuano ya Tenisi ya wazi wa Australia mwaka huu kwa kumchakaza Muhispania Rafael Nadal seti 6-3, 6-2, 6-3.

    katika rekodi, Novak anakuwa mchezaji wa kwanza wa kiume kuchukua ubingwa wa michuano hiyo mara 7 akiwazidi Roy Emerson na Roger Federer.

    Novak kwa sasa ndiye mchezaji wa tenesi namba 1 duniani kwa ubora kwa upande wa wanaume, na ushindi huo unamfanya kufikisha mataji 15 katika maisha yake ya mchezo huo.

    kwa upande wa wanawake, nyota mpya wa tenisi duniani Naomi Osaka raia wa Japan ametwaa taji la michuano hiyo baada ya kumchapa Petra Kvitova wa Jamhuri ya Czech.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako