• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi Afrika Kusini wakamata madereva kumi wa teksi baada ya tukio la ufyatuaji risasi

    (GMT+08:00) 2019-01-28 08:42:19

    Polisi nchini Afrika Kusini wamewakamata madereva kumi wa teksi na silaha zao baada ya tukio ya ufyatuaji risasi kutokea.

    Kwa mujibu wa polisi, Ijumaa iliyopita, shirikisho moja la teksi lilikodi magari ya ulinzi kusindikiza teksi zao zilizokuwa zikitoa huduma kwenye eneo lenye mgogoro. Baadaye, magari hayo yaliyokuwa yanalindwa yalifukuzwa na kundi la watu wanaoshukiwa kuwa ni wanachama wa shirikisho lingine la teksi, na walinzi wao walifyatulia risasi teksi zilizokuwa zikiwafukuza na watu watatu walijeruhiwa vibaya kwa risasi.

    Msemaji wa polisi mkoani Limpopo Bw. Moatshe Ngoepe amelaani vitendo vya kimabavu kwenye sekta ya huduma ya teksi, na kuwahimiza wahusika wajisalimishe kwa mamlaka husika ili kutatua masuala yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako