• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yahimiza ufunguaji mlango kwenye kiwango cha juu zaidi kwa njia ya uoanishaji wa mifumo

  (GMT+08:00) 2019-01-28 16:24:37

  Katika Mkutano wa mwaka 2019 wa Baraza la Uchumi Duniani WEF uliofanyika wiki iliyopita, China imeonesha kwa mara nyingine tena nia na imani ya kusukuma mbele kwa pande zote ufunguaji mlango kwa nje. Katika mwezi mmoja uliopita, mkutano wa kazi ya uchumi wa Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China umetangaza kwa mara ya kwanza kuwa, itahimiza ufunguaji mlango wa kimfumo kutoka kwenye sekta za bidhaa. Hayo yote yanamaanisha kuwa ufunguaji mlango wa China kwa nje utaingia kwenye kipindi kipya.

  Katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, China imekuwa ikivutia raslimali za uzalishaji kutoka nje kutokana na sifa zake za raslimali watu, ardhi na nafasi kubwa ya soko, na kutimiza maendeleo makubwa ya utandawazi wa viwanda na miji. Lakini hivi sasa ongezeko la uchumi la China likitaka kufikia kiwango cha juu zaidi, linahitaji kuundwa kwa mfumo unaoweza kutimiza mawasiliano kati ya raslimali za uchumi kati ya soko la ndani na la nje, na mfumo huo ni msingi muhimu wa kufungua mlango zaidi na kupata maendeleo mapya.

  Hivi sasa ufunguaji mlango wa kimfumo na ushirikiano wa kimataifa ni mwelekeo muhimu wa maendeleo kwa ufunguaji mlango wa uchumi katika kipindi kipya. Ufunguaji mlango wa kimfumo utasaidia kupunguza gharama za biashara chini ya utaratibu wa soko, na pia utasaidia kutimiza mawasiliano ya raslimali za soko la ndani na la nje. China pia imefanya juhudi mbalimbali katika kulinganisha mifumo muhimu ya kimataifa katika sekta ya utungaji wa sera. Kutokana na takwimu mpya zilizotangazwa mwishoni mwa mwaka 2018, uwezo wa ushindani wa mazingira ya biashara ya China umepanda kwa nafasi 32 ukilinganishwa na mwaka uliopita.

  China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, vilevile imekuwa kigezo kipya katika mchakato wa soko la kimataifa, na nchi nyingi zaidi zinazoendelea zimeanza kuzingatia sera za mageuzi za China zinazoelekeza ongezeko la kasi la uchumi, na kutafuta sera zao zenyewe za mageuzi na ufunguaji mlango pamoja na mikakati ya viwanda. Pendekezo na ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" vya China vitakuwa jukwaa jipya la ushirikiano wa kimfumo wa China na nje, ambavyo vitasukuma mbele ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako