• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi wanachama 76 wa WTO ikiwemo China zathibitisha kuanzisha mjadala kuhusu ajenda ya biashara ya kielektroniki

    (GMT+08:00) 2019-01-28 19:23:40

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, nchi wanachama 76 wa Shirika la Biashara la Dunia WTO ikiwemo China zimethibitisha kuanzisha mjadala kuhusu ajenda ya biashara ya kielektroniki, ikiwa ni ishara ya kidhahiri kwa nje.

    Katika mkutano usio rasmi wa mawaziri kuhusu biashara ya kielektroniki uliofanyika huko Davos, nchi hizo zimesaini taarifa ya pamoja ikithibitisha kuanzisha mjadala wa ajenda ya biashara ya kielektroniki.

    Bw. Geng amesema, nchi nyingi wanachama wa WTO zinaunga mkono mfumo wa biashara ya pande nyingi, na kufanya juhudi kulinda mfumo huo wenye msingi wa kanuni na kiini cha WTO, huku wakitumai mfumo huo utaendelea kuhimiza ukuaji wa biashara ya dunia na kutoa mchango katika maendeleo ya uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako