• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapanga kuzindua mfumo wa mabasi ya mwendokasi BRT mwezi Februari

    (GMT+08:00) 2019-01-29 08:38:57

    Kenya inapanga kuzindua mfumo wa mabasi ya mwendokasi BRT mjini Nairobi mwezi Februari, ili kupunguza msongamano wa magari ambao umeleta hasara kubwa kiuchumi, kuchafua hewa na kuathiri afya ya watu.

    Waziri wa uchukuzi, miundombinu, nyumba na maendeleo ya miji Bw. James Macharia amesema serikali iko kwenye mchakato wa kununua kundi la kwanza la mabasi 64 ambayo yametengenezwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya usafiri wa umma mjini Nairobi na katika miji ya karibu.

    Bw. Macharia amedokeza kuwa serikali ya Kenya imetuma timu nchini Afrika Kusini ambako mabasi hayo 64 yatatengenezwa, ili kutathmini viwango vya kiufundi vya mabasi hayo.

    Waziri huyo amesema serikali itawekeza katika marekebisho ya miundombinu ya miji ili kutandika njia kwa ajili ya ujenzi wa BRT kote nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako