• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yaweka vikwazo dhidi ya kampuni ya mafuta ya serikali ya Venezuela

    (GMT+08:00) 2019-01-29 14:02:37

    Marekani imeiwekea vikwazo kampuni moja ya mafuta inayomilikiwa na serikali ya Venezuela. Mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani Bw. John Bolton amesema vikwazo hivyo dhidi ya kampuni ya PDVSA vitazuia mali zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 7 na vinaweza kuisababishia hasara ya dola za kimarekani bilioni 11 mwaka ujao. Vikwazo hivyo vimekuja siku kadhaa baada ya Marekani kumtambua kiongozi wa upinzani Bw. Juan Guaido kuwa rais wa muda wa Venezuela na kumkosoa aliyeko madarakani rais Nicolas Maduro aliyeshinda uchaguzi mwaka jana kwa kupata zaidi ya theluthi mbili ya kura.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako