• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapiga hatua muhimu katika kuhimiza ufunguaji mlango wa kimfumo

    (GMT+08:00) 2019-01-29 16:58:02

    Bunge la umma la China ambalo ni shirika la utungaji wa sheria la China limeanza kufanya ukaguzi wa mara ya pili kwa Sheria ya uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni kuanzia leo, hatua ambayo imeonesha China inadhamiria kukamilisha na kutangaza mapema sheria hiyo, ambayo pia ni hatua muhimu kwa China kufanya ufunguaji mlango wa kimfumo.

    Mwishoni mwa mwaka jana, China ilipoweka mipango ya kazi ya uchumi kwa mwaka 2019, ilisisitiza kuhimiza mabadiliko ya ufunguaji mlango kutoka kwenye bidhaa hadi mifumo, kulegeza masharti ya kuidhinishwa kwenye masoko, kulinda haki halali ya wafanyabiashara wa kigeni nchini China hususan hakimiliki ya ujuzi, na kuruhusu uwekezaji wa kigeni kipekee katika sekta nyingi zaidi.

    Kiini cha ufunguaji mlango wa kimfumo ni kulinganisha mifumo ya kimataifa, na sheria za soko zinazotumika katika kundi kubwa la kiuchumi duniani. Kwa mujibu wa mswada wa Sheria ya uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni, wafanyabiashara wa kigeni wakifanya uwekezaji katika sekta zisizohusishwa kwenye orodha za maeneo yasiyofaa kufunguliwa mlango, watapewa haki kama raia wa China katika kipindi cha kuanzisha biashara na kupata maendeleo na kupanua biashara zao. Mswada huo umetoa thibitisho la kisheria kwa kiwango na uwazi wa mazingira ya uwekezaji nchini China.

    Wachambuzi wameeleza kuwa, kutokana na utaratibu wa upande mmoja, kujilinda kibiashara na athari mbalimbali zisizoweza kutabirika, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje umepungua kwa asilimia 40 katika nusu ya kwanza ya mwaka jana, uwekezaji huo wa nchi zilizoendelea ulipungua kwa asilimia 70, wakati matumizi ya uwekezaji wa kigeni ya China yalizidi RMB yuan bilioni 880, sawa na dola za kimarekani bilioni 131, ambayo ni rekodi mpya katika historia. Kampuni kubwa za Marekani na Ujerumani Tesla na BMW zimeongeza uwekezaji nchini China.

    Kutokana na hali hii, China inatangaza sheria ya uwekezaji kutoka kwa wafanyabiashara wa kigeni si kama tu imeihakikisha China inaweza kuhimiza ufunguaji mlango kwenye kiwango cha juu zaidi kwa kufuata sheria, bali pia inasaidia kuongeza imani ya uwekezaji wa kigeni kuingia kwenye soko la China. Na China inatazamiwa kuendelea kuwa moja kati ya masoko yanayovutia zaidi uwekezaji wa kigeni duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako