• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kufungwa kwa idara za serikali ya Marekani kwasababisha hasara ya dola bilioni 11 za kimarekani

    (GMT+08:00) 2019-01-29 18:18:41

    Ripoti iliyotolewa na Ofisi ya bajeti ya bunge la Marekani imesema, kufungwa kwa baadhi ya idara za serikali ya nchi hiyo tangu Desemba 22 mwaka 2018 hadi Januari 25 mwaka huu kunakadiriwa kuleta hasara ya dola bilioni 11 za kimarekani.

    Ripoti hiyo imesema, kufungwa kwa idara hizo pia kunaweza kusababisha hasara ya asilimia 0.2 ya pato hilo la robo ya kwanza ya mwaka huu yenye thamani ya dola bilioni 8 za kimarekani.

    Kwa mujibu wa kadirio la ofisi hiyo, kufuatia serikali kurejea kazini, uchumi wa nchi hiyo unatarajiwa kurudi katika hali ya kawaida, lakini hasara ya dola bilioni 30 za kimarekani haitarejeshwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako