• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Zaidi ya wafanyabiashara 1500 wa Afrika kukutana mjini Kigali

    (GMT+08:00) 2019-01-29 19:41:45

    Zaidi ya wafanyabiashara 1500 wa kutoka Afrika wanatarajiwa kukutana mjini Kigali mwezi Machi ili kujadili ushirikiano wa kiuchumi wa Afrika.

    Washiriki watajumuisha watunga sera kutoka sekta za viwanda, fedha na siasa, kutoka nchi zaidi ya 70 kujadili ushirikiano wa kikanda pamoja na mada mengine muhimu kwa maendeleo ya biashara za Afrika.

    Mkutano huo wa awamu ya saba kwa jina "Africa CEO Forum 2019", unaleta pamoja viongozi wa biashara na pia utafanya maamuzi kuhusu maswala ibuka ya kibiashara.

    Mkutano huo unakuja wakati ambapo biashara baina ya nchi za Afrika inaendelea kuwa dhaifu unalenga kuwahimiza viongozi wa biashara wenye ushawishi mkubwa barani Afrika kubadilisha hali ya sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako