Michuano ya kombe la Asia imeendelea jana, kwa mchezo wa pili wa nusu fainali baina ya timu ya Qatar kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu, na kufanikiwa kuungana na Japan.
Fainali sasa itazikutanisha Japan na Qatar mchezo utakaochezwa Februari mosi mwaka huu.