• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waethiopia 276 wakamatwa kwa kuhusika na vurugu

  (GMT+08:00) 2019-01-30 09:07:18

  Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa watu 276 wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha kwenye vurugu zilizosababisha vifo mjini Dire Dawa, mashariki mwa Ethiopia.

  Kamati ya polisi ya mji wa Dire Dawa imetoa taarifa ikisema watu 276 wamekamatwa kwa kuhusika na vurugu zilizotokea wiki iliyopita, na polisi wamechukua hatua ili kutuliza hali mjini humo.

  Shuhuda amesema vurugu hizo zilisababishwa na kukosokana kwa usawa katika mpango wa kugawana madaraka kati ya makabila tofauti mjini Dire Dawa. Na vurugu hizo zimesababisha vifo vya watu wasiopungua wawili, na wengine makumi wamejeruhiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako