• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wahamiaji 130 hawajulikani walipo baada ya meli mbili kuzama katika pwani ya Djibouti

  (GMT+08:00) 2019-01-30 18:32:06

  Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema, zaidi ya wahamiaji 130 hawajulikani walipo baada ya meli mbili zilizobeba wahamiaji kupinduka katika pwani ya Djibouti.

  Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema, meli hizo zimezama jana asubuhi, muda mfupi baada ya kuingia kwenye Bahari Nyekundu, na kuongeza kuwa, mpaka sasa wahamiaji wawili wameokolewa na miili mitatu ya wanawake na miwili ya wanaume imepatikana.

  Shirika hilo limesema operesheni ya uokoaji bado inaendelea ili kupata miili ya wahamiaji ambao hawajulikani waliko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako