• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Somalia na UM waahidi kuimarisha uhusiano katika ujenzi wa nchi hiyo

  (GMT+08:00) 2019-01-31 08:34:01

  Somalia na Umoja wa mataifa wamekubaliana kuimarisha uhusiano kati yao unaolenga kuleta mabadiliko katika nchi hiyo.

  Alipofanya mazungumzo na naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia masuala ya siasa na ujenzi wa amani Bibi Rosemary DiCarlo, ambaye yuko ziarani nchini Somalia, rais Mohammed Abdullahi wa nchi hiyo ameahidi kushirikiana kwa karibu zaidi na Umoja wa mataifa ili kuunga mkono ujenzi wa taifa na ujenzi wa amani nchini Somalia.

  Kwenye mazungumzo yao ambayo pia yalihudhuriwa na waziri mkuu wa Somalia Bw. Hassan Ali Khaire, viongozi hao watatu walijadili hatua za kiutendaji zitakazochukuliwa na serikali ya Somalia na Umoja wa mataifa kuimarisha ushirikiano kati yao kwa ajili ya maslahi ya wasomali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako