Waziri Mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May na kiongozi wa chama cha Leba Bw. Jeremy Corbyn wamefanya mazungumzo ya kwanza kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya.
Msemaji wa Bw. Corbyn amesema pande mbili zimefanya mazungumzo mazuri kuhusu umoja wa forodha na soko la pamoja, na kusema wanaweza kufanya mazungumzo zaidi baadaye.
Viongozi hao wamekutana wakati Umoja wa Ulaya unajiandaa na Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya bila kuwa na makubaliano kuhusu ushirikiano kati ya pande mbili. Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean-Claude Junker ameuambia Umoja wa Ulaya kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa Uingereza kujitoa bila kuwa na makubaliano yoyote.
Bw. Junker na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo ya Brexit Bw. Michel Barnier wamesema kwenye bunge la Umoja wa Ulaya kuwa watakataa juhudi za Uingereza kutaka kujadili upya suala la mpaka wa Ireland.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |