Spika wa Bunge la umma la China Bw. Li Zhanshu amekutana na Emir wa Qatar Tamim Bin Hamad Al-Thani katika jumba la mikutano ya umma mjini Beijing.
Bw. Li amesema, bunge la China lina nia ya kushirikiana na bunge la Qatar katika kutekeleza makubaliano muhimu kati ya Rais Xi Jinping na Emir wa Qatar, kuimarisha mawasiliano katika mambo ya utungaji wa sheria, na kukuza kwa pamoja mpango wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ili kuunda mazingira nzuri ya kisheria ya nishati, miundombinu, uwekezaji na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake, Bw. Tamim amesema Qatar inazingatia kuendeleza uhusiano wa kiwenzi wa kimakakati na China, na kutarajia kuimarisha kupanua ushirikiano wa nchi hizo mbili katika sekta ya biashara, michezo na utalii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |