• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gazeti la Renminribao latoa ripoti mfululizo kuhusu tamasha la mwaka mpya wa jadi wa kichina la CCTV

    (GMT+08:00) 2019-01-31 18:58:36

    Hivi karibuni gazeti la Renminribao limetoa ripoti mfululizo kuhusu tamasha la mwaka mpya wa jadi wa kichina litakaloandaliwa na Shirika kuu la Utangazaji la China CMG.

    Habari zilizotolewa na gazeti hilo zinasema, likiwa tamasha la kwanza tangu CMG izinduliwe, tamasha hilo lenye kauli mbiu ya "kujiendeleza katika zama mpya, na kusherehekea mwaka mpya wenye baraka" litakuwa na maonesho mazuri ya nyimbo, ngoma, opera za kichina, michezo mifupi ya kuigiza na mazungumzo ya kuchekesha.

    Mwaka huu tamasha hilo litaoneshwa kwa mara ya kwanza kupitia majukwaa mbalimbali, ikiwemo televisheni, radio, APP na mitandao ya kijamii, na teknolojia ya 5G pia itatumiwa kwa mara ya kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako