• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa UM apongeza ajenda ya mageuzi Somalia

    (GMT+08:00) 2019-02-01 08:27:51

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia masuala ya siasa na ujenzi wa amani, Bibi Rosemary DiCarlo amemaliza ziara yake ye siku mbili nchini Somalia, akiipongeza serikali ya Somalia kwa ajenda yake ya mageuzi yanayoendelea.

    Bibi DiCarlo amesisitiza uungaji mkono thabiti wa Umoja wa mataifa kwa utekelezaji wa hatua muhimu zinazochukuliwa na serikali ya Somalia kwenye nyanja za siasa shirikishi, usalama na haki, ufufuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii.

    Bibi DiCarlo ametoa wito kwa viongozi wa Somalia kutoa kipaumbele katika utawala bora, haki za binadamu hasa za wanawake, na kukamilisha mapitio ya kikatiba.

    Ofisa huyo amesema wakati Somalia inapokaribia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, Umoja wa mataifa uko tayari kuendelea kuiunga mkono Somalia na watu wake katika kutimiza malengo yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako