• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasimamizi wa mambo ya nishati barani Afrika wasaini makubaliano na wenzao wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2019-02-01 08:43:05

    Wasimamizi wa nishati wa nchi za mashariki na kusini wa Afrika wamesaini makubaliano ya ushirikiano na wenzao wa Ulaya, wenye lengo la kubadilishana uzoefu kwenye kazi zao.

    Jumuiya ya wasimamizi wa nishati kwenye nchi za Mashariki na kusini mwa Afrika (RAERESA) na baraza la wasimamizi wa nishati la Ulaya (CEER) wamesaini makubaliano ya miaka mitatu, yatakayosimamiwa na soko la pamoja la nchi za mashariki na kusini mwa Afrika COMESA.

    Makubaliano hayo pia yanalenga kufanikisha ujenzi wa uwezo kwenye eneo la mashariki na kusini mwa Afrika, kupitia kueneza uzoefu mzuri wa kazi.

    Maeneo ya msingi ya ushirikiano ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa kitaasisi na mamlaka. Kubadilishana ujuzi na kuhimiza ushindani kwenye masoko ya nishati ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako