• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Cavaliers yainyuka Bulls, Hutchinson kuwa nje kwa mwezi mzima

    (GMT+08:00) 2019-02-01 09:00:15
    Jordan Clarkson na Alec Burks kila mmoja alifunga pointi 18, Cedi Osman akaongeza 17 na Cleveland Cavaliers ikamaliza mwendo wa kupoteza michezo sita mfululizo kwa kuichapa Chicago Bulls 104-101, katika ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani (NBA).

    Hadi sasa Bulls imepoteza mechi tatu mfululizo, na itamkosa mchezaji wake mahiri Rookie Chandler Hutchinson aliyeumia mfupa wa mguu wa kulia katika mechi ya alhamisi iliyopita na imefahamika sasa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako