Shirika la habari la Syria SANA limesema, jeshi la Marekani na kikosi cha SDF kinachoungwa mkono na jeshi hilo limezuia msafara wa malori ya serikali ya Syria yanayosafirisha vitu vya msaada kuingia katika wilaya ya Hajin mkoani Deir al-Zour, mashariki mwa nchi hiyo.
Shirika hilo limesema, msafara huo uliobeba maji ya kunywa, dawa, na vifaa vya usafi ulizuiwa na kikosi cha SDF kinachoongozwa na kundi la Wakurdi na kuarifiwa kuwa jeshi la Marekani limepiga marufuku msafara huo kuingia wilayani Hajin.
SANA limelaani kitendo hicho cha jeshi la Marekani na kikosi cha SDF, na kusema kimekiuka sheria ya kimataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |