• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadukuzi wezi wa benki 130 wasakwa Kenya

    (GMT+08:00) 2019-02-01 18:44:00
    Idara ya upelelezi nchini Kenya DCI imechapisha majina ya watu 130 ambao wanawindwa na polisi, kwa makosa ya kudukua mitambo ya benki.

    Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii na kurasa saba za magazeti ya Kenya , idara hiyo ilichapisha majina, sura na nambari za vitambulisho za washukiwa hao, huku ikiwataka watu kupiga ripoti kwa polisi wanapowaona.

    Wachunguzi hao wa makosa ya jinai aidha walitoa nambari za simu ambazo watu wanaweza kuripoti kwa kupiga simu ama kutuma jumbe fupi.

    Idara ya DCI aidha ilisema kuwa ilipokea amri kutoka mahakama za Kiambu na Milimani kuwakamata washukiwa hao.

    Orodha hiyo vilevile ina wanawake 30, kati ya washukiwa hao 130.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako