• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China awatembelea wakazi wa Beijing kabla ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China

    (GMT+08:00) 2019-02-02 09:10:39

    Rais Xi Jinping wa China aliwatembelea watumishi na wakazi jana hapa Beijing, na kutoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China kwa watu wa makabila mbalimbali nchini China.

    Jana asubuhi rais Xi Jinping alitembelea kwanza idara ya polisi ya mji wa Beijing, na kuongea na polisi walioko kazini kwa njia ya video.

    Baadaye rais Xi alikwenda kuwatembelea wakazi wa barabara ya Caochang Sitiao Hutong mashariki mwa mtaa wa Qianmen. Alitengeneza chakula cha jadi cha kichina kiitwacho Jiaozi pamoja na wakazi wa kule, na kutoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China kwa watu wote, akisema,

    "Ningependa kuchukua fursa hii kutoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China kwa watumisi na wakazi wote wa mji wa Beijing, na watu wa makabila mbalimbali nchini China! Nawatakia watu wote kupata maisha bora zaidi, naitakia nchi yetu istawi zaidi! Nawatakia maisha yenye masikilizano, kazi njema na heri ya mwaka mpya!

    Kabla ya kuondoka kutoka mtaa wa Qianmen, rais Xi aliwatembelea wafanyakazi wa kituo cha kupeleka mizigo cha barabara ya Shitou Hutong, na alitembelea mgahama mdogo na kuongea mmiliki wa mgahawa huo.

    Jana mchana rais Xi Jinping alitembelea kituo cha maonesho na ofisi ya michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing na kituo cha michezo ya majira ya baridi katika eneo la Shijingshan, ili kukagua kazi ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki na michezo ya Olimpiki ya walemavu ya majira ya baridi itakayofanyika mwaka 2022 hapa Beijing, na kutoa salamu za mwaka mpya kwa wafanyakazi, wachezaji na kocha wa michezo hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako