• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pande zenye mgogoro nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR zafikia makubaliano ya amani

    (GMT+08:00) 2019-02-03 19:07:01

    Wawakilishi wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na pande zenye mgogoro jana wamefikia makubaliano ya amani huko Khartoum, nchini Sudan.

    Likimnukuu mkuu wa mazungumzo wa upande wa Sudan Bw. Attal-Mannan Bakheet, Shirika la Habari la Sudan limesema kuwa mambo makuu waliyokuwa wakitofautiana kwenye mazungumzo hayo ni pamoja na, kugawana madaraka, utekelezaji wa sheria katika kipindi cha mpito, na masuala mengine.

    Bw. Bakheet amesema kuwa rasimu ya makubaliano kwanza itasainiwa leo mbele ya marais wa Sudan na Jamhuri ya Afrika ya Kati , na makubaliano ya mwisho ya amani yatasainiwa Jumatano ijayo huko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako