• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China

    (GMT+08:00) 2019-02-03 20:55:36

    Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China na baraza la serikali la China leo zimeandaa tafrija ya kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China. Kwenye tafrija hiyo, Rais Xi Jinping wa China amehutubia, na kutoa salamu za mwaka mpya kwa wananchi wa makabila mbalimbali kote nchini, ndugu wa Hongkong, Macao, Taiwan na wachina wanaoishi nchi za nje.

    Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, katika mwaka uliopita, uchumi wa China uliendelezwa kwa madhubuti, mambo ya mageuzi na kufungua mlango yamepiga hatua mpya, vita dhidi ya umaskini vimepata mafanikio makubwa, mageuzi ya ulinzi na jeshi yameendelea kuzidishwa, mambo ya kidiplomasia yenye umaalumu wa China yamefungua ukurasa mpya, watu wa China wamepata furaha na salama.

    Pia amesema, tangu enzi na dahari, wachina wanaheshimu wazee, kwa sasa China imeingia kwenye jamii yenye wazee wengi, inapaswa kufanya juhudi kuendeleza mambo yanayohusu wazee, ili wazee wote wawe na maisha mazuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako